HabariMilele FmSwahili

Waziri Karoney aapa kubuni mikakati ya kutatua migogoro ya umiliki wa ardhi nchini

Waziri mpya wa Ardhi Farida Karoney ameapa kubuni mikakati ya kutatua migogoro ya umiliki wa ardhi nchini. Akichukuwa rasmi mamlaka katika wizara hiyo kutoka kwa profesa Jacob Kaimenyi, Karoney amesema atashirikiana na maafisa wizara hiyo pamoja na tume ya kitaifa ya ardhi kushughulikia migogoro iliyopo. Pia waziri huyo amesema atahakikisha mifumo wa kidijitali unaimarishwa katika uhifadhi rekodi pamoja na utoaji hati miliki za ardhi kwa wakati.

Show More

Related Articles