HabariMilele FmSwahili

Keter na washukiwa wenza 2 waachiliwa kwa dhamana ya milioni 2 kila mmoja

Mbunge wa Nandi Hills Alfred Keter pamoja na washukiwa wenza wawili wenza Madat Chatur na Jonhstone Sakwa wamekanusha mashata ya ulaghai na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 2 pesa taslimu kila mmoja. Hakimu wa mahakama ya Milimani Francis Andayi amewaagiza watatu hao kufika katika makao makuu ya idara ya jinai mara moja kwa wiki kusaidia katika uchunguzi. Watatu hao wanatuhumiwa kuwasilisha hati dhamana ghushi za shilingi milioni 633 kwa benki kuu ya Kenya. Kesi itasikilizwa Juni 4.

Show More

Related Articles