HabariMilele FmSwahili

Mawaziri 9 walioapishwa Ijumaa iliyopita kutwaa rasmi yadhifa zao leo

Mawaziri tisa walioapishwa Ijumaa wiki iliyopita wanaanza kutwaa rasmi nyadhifa zao leo. Tayari waziri wa mazingira Keriako Tobiko amechukuwa mamlaka kutoka mtangulizi wake profesa Judy Wakhungu. Wengine wanaochukuwa mamlaka ni waziri mpya wa ardhi Farida Karoney atapokezwa wadhifa huo na waziri anayeondoka profesa Jacob Kaimenyi. Kwengineko waziri anayeondoka wa utumishi wa umma Sicily Kariuki atamkabidhi wadhifa huo profesa Margeret Kobia.

Show More

Related Articles