HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakali Kwanza Watangaza Kuvunjilia Mbali Kundi Hilo

Baadhi ya wananchama wa kundi la wahalifu la wakali kwanza kisauni, wametangaza nia yao ya kujisalimisha na kuwa wanahitaji hakikisho la usalama wao kutoka kwa jamii na vyombo vya usalama kabla ya kufanya hivyo.

Mbunge wa kisauni Ali Mbogo amesema amepokea ujumbe huo kutoka kwa yule anayedaiwa kuwa kiongozi wa kundi hilo la wakali kwanza eneo la kisauni wakisema wako tayari kulivunjilia mbali kundi hilo na kuhubiri amani.

Sasa ofisi ya Mbogo ikishirikiana na ile ya Naibu kamishina kaunti ndogo ya Kisauni zinandaa zoezi la kuwapokea vijana hao kama njia ya kukomesha kabisa utata wa uhalifu ndani ya Kisauni.

Kauli hii inakuja baada ya kamishina wa kaunti ya Mombasa Evans Achoki kuapa kuwa maafisa wa polisi walikuwa wanapanga kuyafeka makundi yote haramu yanayowahangaisha wakaazi ndani ya maeneo mbali mbali ya kaunti mombasa

Show More

Related Articles