HabariMilele FmSwahili

Mbunge wa Nandi hills Alfred Keter akamatwa

Mbunge wa Nandi Hills Alfred Keter amematwa kuhusiana na tuhuma za kughushi hati dhamana maarufu treasuary bills kutoka kwa benki kuu. Inadaiwa Keter alighushi stakabadhi hizo ili kupokea shilingi milioni 633. Kwa mujibu wa afisa wa mawasiliano katika benki kuu Wallace Kantai Keter amekamatwa pamoja na washukiwa wengine wawili Madat Chatur na Arthur Sakwa ambao ni wakurugenzi wa kampuni ya Desai Industies. Hata hivyo Keter amedai kuwajuza maafisa kuhusu stakabadhi hizo na wala hana hatia.

Show More

Related Articles