HabariPilipili FmPilipili FM News

Kilimo Mambo Leo; Taita Taveta

Wakulima na wafugaji kaunti ya Taita Taveta wamepangwa kuimarisha mazao, baada ya shirika la umoja wa kimataifa US-AID kuiorodhisha kaunti hiyo miongoni mwa kaunti 12 zitakazofaidika na mradi wa miaka mitano wa FEED THE FUTURE

Naibu mkurugenzi wa shirika la US-AID chini ya mpango huo dakitari Rita Laker-Ojok , amesema hatua hiyo iliafikiwa baada ya wao kukubaliwa na nchi ya marekani , akiongeza kuwa mradi huo  unalenga kuongeza uzalishaji na kuboresha mazao, ili kubuni nafasi za ajira.

Kulingana naye kaunti hiyo ni ya pekee kuorodheshwa kwa mradi huo pwani, licha ya makao yake makuu kuwekwa mjini Wotee eneo la ukambani kuzihudumia kaunti za Makueni , Kitui na Taita Taveta.

Kwa upande wake Gavanawa kaunti hiyo  Granton Samboja ameomba miradi itakayoanzishwa kuwa ya kudumu na yenye faida  kwa wanainchi katika juhudi za kukabili umasikini.

Kaunti zingine zitakazofaidika na mradi huo ni Kitui, Makueni, Homabay, Migori, Kisii, Kisumu, Siaya, Kakamega, Busia,Bungoma na Vihiga.

 

Show More

Related Articles