HabariPilipili FmPilipili FM News

Mawaziri Tisa Walio Pendekezwa Wapishwa Rasmi katika ikulu ya Rais

Rais Uhuru Kenyatta leo ameongoza hafla ya kuwalisha kiapo rasmi mawaziri 9 wapya walioteuliwa katika baraza lake la mawaziri.

Miongoni mwa mawaziri walioapishwa hii leo ni Mageret Kobia waziri wa utumishi wa umma,John Munyesh wa madini,keriako tobiko wa mazingira,Farida Karoney wa  ardhi,Rashid Achesa Michezo, Ukur Yattani waziri wa leba, pamoja na Peter Munya waziri wa jumuiya ya Afrika mashariki.

Wengine ni Monica Juma waziri wa masuala ya nje pamoja na Samuel Chelugui anaye chukua wizara ya maji.

Akiongea wakati wa hafla hiyo iliyofanyika Katika ikulu ya rais jijini Nairobi, Rais Uhuru Kenyatta amewahimiza mawaziri hao wapya kuzingatia majukumu yao mapya, na kujitolea katika kuwahudumia wakenya wote kwa usawa.

 

Show More

Related Articles