HabariMilele FmSwahili

Mawaziri 9 walioidhinishwa na bunge waapishwa

Mawaziri tisa walioidhinishwa na bunge wiki hii wameapishwa wakati katika ikuli ya Nairobi. Wakwanza kula kiapo amekuwa waziri wa utumishi ya umma Margeret Kobia akifuatiwa na John Munyes wa madini. wa tatu amekuwa waziri wa mambo ya kigeni Monica Juma. Keriako Tobiko aliyechaguliwa kuwa waziri wa mazingira amekuwa wa nne kuapishwa, Simon Chelugui wa maji akifuatia. Rashid Echesa Mohamed amekuwa waziri wa sita kuapishwa akifuatiwa na Faridah Karoney. Ukur Yatanni wa leba amekuwa wa nane naye waziri wa jumuiya ya afrika mashariki Peter Munya amekuwa wa mwisho.

Show More

Related Articles