HabariPilipili FmPilipili FM News

Wanawake Waongoza Kwa Kujiunga Na Makundi Ya Ugaidi

Kaunti ya Mombasa ,kwale na Lamu zimeorodheshwa kuongoza Kwa idadi ya wanawake wanaojiunga na makundi ya ugaidi. Haya ni kulingana na shirika lisilo la kiserekali la ACT Kwa ushirikiano na shirika la US-AID.

Meneja wa ujenzi wa mipango  ya amani wa  shirika la ACT kanda ya pwani Dominic Pkalya, ameeleza kuwa ongezeko hili limesababishwa na ukosefu wa ajira, pale vijana wanapokosa mambo ya kujishughulisha nayo, shinikizo la watu wenye rika moja, pamoja na ukosefu wa elimu ya usawa kuhusiana na dini.

Show More

Related Articles