HabariMilele FmSwahili

Vikao vya kupokea ushahidi kuhusiana na mauaji ya mtoto pendo kuanza leo Kisumu

Vikao vya kupokea ushahidi wa umma kuhusiana na mauaji ya mtoto Pendo vinatarajiwa kuanza leo katika mahakama kuu mjini Kisumu. Kesi hiyo inayosiklizwa na Hakimu Beryl Omollo iliahirishwa kutoka Januari Nane. Aliyekuwa kiongozi wa mashitaka ya umma Keriako Tobiko aliagiza vikao hivyo kufanyika kwa lengo la kuwachukulia hatua maafisa wa polisi wanaodaiwa kutekeleza mauaji hayo. Mtoto Pendo alidaiwa kupigwa na maafisa wa polisi nymbani kwao mjini Kisumu wakati wa maandamano baada ya uchaguzi wa Agosti Nane mwaka jana.

Show More

Related Articles