People Daily

Mawaziri Waliopendekezwa Kuapishwa Rasmi Leo

Mawaziri waliopendekezwa kuhudumu katika baraza la mawaziri na kukaguliwa na kamati ya uteuzi bungeni, wanatarajiwa kuapishwa rasmi hii leo.

Hii ni baada ya kamati ya bunge kuhusu uteuzi, kujadili na kuidhinisha wote 9 walioteuliwa na rais Uhuru Kenyatta.

Wabunge wa jubilee kwa pamoja waliunga mkono ripoti ya ukaguzi kuhusu 9 hao hata licha ya wabunge wa NASA kususia vikao vya kujadili ripoti hiyo.

Kati ya Tisa hao ni Magerete Kobia aliyependekezwa kusimamia wizara ya utumishi wa umma, John Munyes wizara ya madini, Keriako Tobiko wizara ya mazingira, Faridah Karoney Wizara ya ardhi, Rashid Achesa Michezo, Ukur Yatani wizara ya leba ,pamoja na Peter Munya katika Wizara mpya  ya jumuiya ya Afrika mashariki.

Show More

Related Articles