HabariMilele FmSwahili

Samuel Kimaru sasa ndiye kamanda wa trafiki nchini

Samuel Kimaru sasa ndiye kamanda wa trafiki nchini. Anachukua nafasi hiyo kutoka kwa Jacinta Muthoni. Katika mabadiliko yaliotekelezwa na naibu inspecta generali wa polisi Edward Mbugua Joseph Lle Tito ndiye kamanda wa polisi Nairobi akichukua pahala pa Japheth Koome ambaye sasa atahudumu kama naibu inspecta generali wa polisi. Kingori Mwangi ambaye hadi leo amehudumu kama naibu katibu wa inspecta generali sasa ndiye kamanda wa chuo cha mafunzo cha Kiganjo. Sarah Duncan kamanda wa polisi huko Siasa amehamishwa hadi makao makuu ya polisi miongoini mwa wengine.

Show More

Related Articles