HabariPilipili FmPilipili FM News

Mawakili Washinikiza Serikali Kutii Maagizo Ya Mahakama.

Chama cha mawakili nchini LSK tawi la Mombasa kimehairisha kampeni yake ya kutaka  serikali na wananchi kwa ujumla kuheshimu sheria za mahakama.

Mwenyekiti wa chama hicho kaunti ya Mombasa Matthew Nyabena amesema imewalazimu kuhairisha kampeni hiyo kufuatia kifo cha mmoja wao kilichotokea wiki hii.

Hata hivyo amesema kampeni hiyo bado itaendelea, lengo kuu ikiwa ni kuhakikisha kila Mkenya anafuata sheria na maagizo ya mahakama.

Hata hivyo Tayari Kampeni hiyo ya utepe wa njano imeng’oa nanga katika kaunti za Nairobi na kisumu ambapo mwenyekiti wa chama mawakili nchini LSK tawi la kisumu Samuel Onyango amesisitiza kuwa ni lazima maamuzi na sheria za mahakama ziheshimiwe.

Mawakili walipania kususia vikao vyote vya mahakama leo na kujifunga tepe za njano, kuashiria mwanzo wa kususia utoaji huduma zao, iwapo mtindo unaoendelea wa kutotii sheria na maagizo ya mahakama utaendelea.

 

Show More

Related Articles