HabariPilipili FmPilipili FM News

Kenya Yaweka Mikataba Ya Kisheria Na Serikali Ya Uswizi

Serikali ya Kenya imeweka mkataba wa kisheria na serikali ya uswizi ili kukabiliana na ufisadi pamoja na ufujaji wa fedha za umma.

Akiongea katika mkutano uliowaleta pamoja wakuu wa serikali ya Kenya na uswizi mwanasheria mkuu humu nchini Githu Muigai amesema serikali ya Kenya imeanza uchunguzi wa kurudishiwa fedha zilizofichwa nchini humo.

Wakati huo huo ameishukuru serikali ya uswizi kwa ushirikiano wake mwema wa kusaidia Kenya katika uchunguzi.

Show More

Related Articles