HabariPilipili FmPilipili FM News

Miguna Alipelekwa Canada Kinyume Cha Sheria Yasema Mahakama.

Mahakama kuu jijini Nairobi imesema hatua ya serikali kumsafirisha mwanasiasa Miguna Miguna nchini Canada ilikuwa kinyume cha sheria.

Jaji wa mahakama hiyo Luka Kimaru, pia ameipa serikali siku 7 kuwasilisha paspoti ya Miguna Miguna, kwa msingi kuwa cheti hicho kilifutiliwa mbali kinyume cha sheria.

Aidha amesema agizo la waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang’I kuhusu kusafirishwa kwa Miguna nchini  Canada lilikuwa kinyume cha sheria.

Aidha kimaru amewaagiza inspekta jenerali wa polisi Joseph Boinet na mkurugenzi wa DCI George Kinoti kuandikia mahakama chini ya siku 7 kwamba wataheshimu sheria na maagizo ya mahakama.

Mawakili wa NASA wakiongozwa na James Orengo na mwenzake Otiende Amolo , wamesifia uamuzi huo wakisema unaendana na katiba na kwamba ni lazima kila mmoja aheshimu sheria za katiba.

 

 

Show More

Related Articles