HabariMilele FmSwahili

Watu 17 wafariki katika shambulio la risasi huko Florida Marekani

Watu 17 wameuawa katika mauaji ya watu wengi yaliyofanywa katika shule moja huko Florida Marekani. Kwa mujibu wa polisi, mtuhumiwa huyo ametajwa kwa jina la Nikolaus Cruz mwenye umri wa miaka 19 na kwamba alikuwa mwanafunzi katika shule hiyo aliyoishambulia. Mshambuliaji huyo ambaye alikuwa amebeba bunduki ya kisasa, alianza kushambulia bila ya mpangilio nje ya shule hiyo kabla ya kushambulia ndani, hali ambayo ilisababisha wanafunzi, kuhangaika huku na kule kwa lengo la kujificha chini ya madawati na maeneo mengine.

 

Show More

Related Articles