HabariMilele FmSwahili

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ajiuzulu

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amejiuzulu baada ya shinikizo nyingi kutoka kwa chama chake.Kapitia hotuba yake iliyopeperushwa kwa njia ya televisheni alisema anajiuzulu mara moja lakini akaongeza kuwa hakubaliani na uamuzi wa chama cha ANC.

Chama cha ANC kilikuwa kimemuambia aondoke madarakani au akabiliwe na kura ya kutokuwa na imani naye bungeni Zuma mwenye umri wa miaka 75 amekuwa akikabiliwa na shinikizo za kumtaka ampe nafasi makamu wake Cyril Ramaphosa, ambaye ndiye sasa kiongozi mpya wa chama.Bw Zuma ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2009, amekumbwa na shutuma nyingi za ufisadi. Mapema Jumatano, polisi walivamia nyumba ya familia tajiri ya Gupta ambayo Zuma ana uhusiano wa karibu nayo.

Show More

Related Articles