HabariMilele FmSwahili

Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai afariki

Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai amefariki Waziri huyo mkuu wa zamani wa Zimbabwe, 65, alikuwa akisumbuliwa na saratani na alikuwa akipata matibabu katika hospitali moja nchini Afrika Kusini. Bw Tsvangirai na chama chake cha Movement for Democratic Change alikuwa akipambana kisiasa na utawala wa rais Robert Mugabe.

Show More

Related Articles