HabariMilele FmSwahili

Mawakili kuandamana kutaka wakenya wote kuheshimu sheria

Mawakili watafanya maandamano kutaka wakenya wote kuheshimu sheria. Mawakili hao watasusia vikao vyote vya mahakama leo na kujifunga tepe za njano kuashiria mwanzo wa kususia utoaji huduma kama hatua ya kulalamika kuhusu mtindo unaoendelea wa kutotii sheria na maagizo ya mahakama. Kampeni hiyo ya utepe wa njano itaendelea hadi pale watu watakapoanza kufuata sheria. LSK imeongeza kuwa mawakili hao watawashtaki maafisa wakuu serikalini na wale wa uma wasiozingatia sheria.

Show More

Related Articles