HabariMilele FmSwahili

Mtoto wa miaka 12 ajitia kitanzi Mai Mahiu

Wenyeji wa Mai Mahiu huko Naivasha wamesalia na mshtuko baada ya mtoto wa darasa la 7 kujitia kitanzi. Mtoto huyo a miaka 12 mwanafunzi katika shule ya msingi ya Ngeya alijiua kwa kujinyonga katika chumba cha kulala cha mamake kulalamikia hatua ya kutenganishwa na babake. Kimani Kamau mmoja wa wenyeji anasema marehemu alimtembelea babake majuma mawili yaliyopita na kuwataka kurejea kuishi na mamake ambaye andai amekuwa akimdhulumu. OCS wa kituo cha polisi cha Mai Mahiu Ezra Sambu anasema wameanzisha uchunguzi kwenye kiini cha mkasa huo.

Show More

Related Articles