HabariMilele FmSwahili

Watu 9 walioidhinishwa kuhudumu kama mawaziri kujua hatma yao leo

Watu 9 walioidhinishwa kuhudumu kama mawaziri wanatazamiwa kubaini hatma yao mchana wa leo baada ya wabunge kujadili ripoti ya kamati ya uteuzi. Iwapo 9 hao wataidhinishwa basi watalishwa kiapo cha kuhudumu moja kwa moja na kuanza rasmi majukumu yao. Upinzani unatazamiwa kususia mjadala huo kwa dai hawatambui uongozi wa rais Uhuru Kenyatta. Wakati huo huo bunge limeidhinisha hoja ya kuongezwa muda wa kujadili ripoti ya kuwaidhinisha waliopendekezwa na rais Uhuru Kenyatta kuhudumu kama makatibu na mabalozi. Wabunge wa Jubilee wamewazidi wale wa NASA kuidhinisha hoja hiyo iliowasilishwa na kiranja wa wengi Benjamin Washiali.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.