HabariMilele FmSwahili

Rais awataka maseneta kuongoza mchakato kuhakikisha ugatuzi unafanikiwa nchini

Rais Uhuru Kenyatta amewataka maseneta kuongoza mchakato wa kuhakikisha ugatuzi unafanikiwa nchini. Akiongea alipokutana na maseneta wa Jubilee katika ikulu ya Nairobi mapema leo, rais Kenyatta amesema ni wajibu wa maseneta kuhakikisha sheria hitajika kuhusu ugatuzi zinapasishwa pasi na mali ya umma kutumiwa visivyo. Rais aliyeandamana na naibu wake William Ruto wanasema serikali inaunga mkono kikamilifu mfumo wa ugatuzi kama njia mojawapo ya kuafikia ajenda kuu nne za serikali yake. Mkutano huo unajiri siku moja baada ya rais na naibu wake kukutana na wabunge wa Jubilee ambapo waliafikiana kuhakikisha ajenda ya serikali.

Show More

Related Articles