HabariPilipili FmPilipili FM News

Wananchi Wa Taita Taveta Waombwa Kuheshimu Viongozi Waliochaguliwa

Wito umetolewa kwa wananchi na viongozi wa kisiasa kaunti ya Taita Taveta kumuunga mkono gavana na viongozi waliochaguliwa katika kaunti hiyo ili kuwezesha ufanisi wa maendeleo katika kaunti hiyo.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara mjini Taveta,mbunge wa eneo hilo Naomi Shaaban ameonekana kuwakosoa  wanaopinga gavana Granton Samboja akisema wakati wa siasa umepita.

Amesema endapo jamii katika kaunti hiyo haitawaheshimu viongozi walioko basi  huenda kaunti hiyo ikasalia nyuma kimaendeleo.

Show More

Related Articles