HabariMilele FmSwahili

Serikali ya kaunti ya Nairobi yakamata mifugo zaidi ya 1000 katikati mwa jiji

Serikali ya kaunti ya Nairobi imewakamata zaidi ya mifugo 1,000 waliopatikana wakitafuta lishe kati kati mwa jiji. Waziri wa mifugo na misitu Danvas Makori anasema mifugo hao wanazuiliwa na watapigwa mnada baada ya siku 7 huku wenyewe wakifungwa jela miezi sita. Aidha ametoa onyo kali kwa wafanyibiashara wanaokata miti kiholela ili kuweka mabango ya matangazo akisema wahusika watakabiliwa vilivyo. Anasema wanaoendesha uharibifu huo watagharamia kung’olewa mabango hayo ya matangazo.

Show More

Related Articles