HabariPilipili FmPilipili FM News

Joto Kali Yatarajiwa Kukumba Nchi Ya Kenya.

Sehemu Mbalimbali nchini zinatarajiwa kukumbwa na  joto kali hatua inayotarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi machi mwaka huu.

Kulingana na ripoti ya  hali ya hewa ya muungano wa mataifa ya IGAD,  vipindi vya joto vilianza mwezi Decemba mwaka jana katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kazkazini mwa nchi.

Akitoa ripoti hiyo Mkurugenzi wa idara ya hali ya hewa nchini Peter Ambenje, amesema Magojwa yatokanayo na uchafu  na vumbi yanatarajiwa Kuongezeka Ukanda wa Pwani ,Mkoa wa kati na Kazkazini mwa nchi .

Ripoti hiyo vilevile  imeeleza kwamba Ugonjwa wa malaria, na utapia mlo, yanatarajiwa kuongezeka  nchini na pia mataifa ya IGAD, katika kipindi cha msimu wa Mvua na Ukame.

Hayo yakijiri Idara ya  hali ya hewa humu nchini inatarajiwa kutoa ripoti yake kamilifu juma lijalo, kubaini idadi ya viwango vya mvua vinavyotarajiwa Kunyesha nchini au iwapo taifa litakumbwa na ukame almaarufu Lanina.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.