HabariPilipili FmPilipili FM News

Naibu Kamishna Eneo La Jomvu Anyooshewa Kidole Cha Lawama

Mbunge wa Jomvu Badi Twalib amemtaka aliyekuwa mshirikishi wa serikali kuu Pwani Nelson Marwa kuingilia kati  na kuhakikisha kuwa kaimu  naibu kamishna eneobunge la Jomvu  Elizabeth Ngava, anachunguzwa kwa kile kinadaiwa kuhusika na unyakuzi wa ardhi eneo hilo.

Hii ni baada ya baadhi ya maafisa wa Polisi wa eneo hilo kupatikana wakisimamia shughuli ya kulima barabara katika kipande cha ardhi, kinachodaiwa kunyakuliwa na bwenyenye mmoja eneo la Miroroni Gotani, Suala ambalo Badi anasema linaibua masuali mengi.

Also read:   Kamati ya bunge kuweka wazi Sheria kuhusu ardhi

Siku chache zilizopita  kiongozi huyo aliwapatia siku 7 mabwenyenye 3 wanaohusishwa na unyakuzi wa ardhi eneo hilo, kuwasilisha hatimiliki ya ardhi zao kwa wizara ya Ardhi kaunti ya Mombasa, la sivyo wakabiliwe kisheria.

Kwa mda sasa unyakuzi wa ardhi umekuwa changamoto kuu kwa wakazi wa kaunti za pwani, huku kaunti za mombasa , kwale na kilifi zikiorodheshwa miongoni mwa kaunti zinazoripoti visa vingi vya unyakuzi wa ardhi.

Also read:   Tume ya polisi yashirikiana na viongozi kuyakomesha,mauaji ya kiholela, Mombasa
Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker