HabariPilipili FmPilipili FM News

Serikali Ya Kaunti Ya Kilifi Ya kana Madai Ya Kuwatenga Walemavu

Siku tatu baada ya watu wanaoishi na ulemavu  kaunti ya Kilifi kulalamikia kutengwa na kudhulumiwa na kaunti hiyo, serikali ya kaunti hiyo sasa imekana madai hayo.

Katibu wa idara ya jinsia, utamaduni na huduma za jamii katika kaunti hiyo Maureen Mwangovya, amesema  serikali ya kaunti hiyo haijawasahau walemavu kwani tayari kuna mpango wa kuwajengea kituo cha biashara, ambapo wao wenyewe waliweza kuhusika katika kutoa maoni ya mpango huo, akiongeza kuwa wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha walemavu wanafaidi kama wengine.

 

Show More

Related Articles