People Daily

Eneo la Kisauni La Orodheshwa Miongoni Mwa Maeneo Hatari Kwa Usalama

Idara ya polisi kaunti ya Mombasa imeliorodhesha eneo la kisauni kuwa miongoni mwa maeneo yaliyokithiri visa vya uhalifu katika siku za hivi karibuni.

Hayo ni kwa mujibu wa kamanda wa polisi kaunti ya Mombasa Johnstone Ipara, wakati akitoa ripoti ya idara hiyo kuhusu hali ya usalama mjini Mombasa.

Ipara anasema kufikia sasa zaidi ya watu 20 wengi wao wakiwa vijana wanaohusishwa na makundi ya uhalifu wametiwa mbaroni na kufikishwa mahakamani.

Ipara aidha amewahakikishia wakazi wa mombasa kwamba polisi wanafanya kila wawezalo kuyakabili makundi ya uhalifu, yanayohangaisha wananchi, huku akihimiza viongozi na wananchi kudumisha ushirikiano mzuri baina yao na asasi za usalama

Show More

Related Articles