People Daily

KNUT Ya Taka Walimu Kupewa Elimu Ya Kutosha Kuhusiana Na Mfumo Mpya Wa Elimu

Chama cha walimu nchini KNUT kimeitaka serikali kutouharakisha mfumo mpya wa elimu na badala yake  kuwapa fursa walimu kuufahamu vizuri mfumo huo.

Akizungumza katika shule ya msingi ya Kilifi ,naibu wa katibu mkuu wa chama hicho Hezbon Otieno ameitaka serikali kuanza kuutumia mfumo huo rasmi, baada ya mwaka 2019 pindi walimu watakapokuwa wamejifahamisha vyakutosha kuhusu  mfumo huo.

Wakati uo huo ametoa wito kwa tume ya kuwaajiri walimu nchini TSC kuendeleza shughuli yao ya kuwapandisha vyeo walimu, ambayo anasema imekwama tangu mwaka 2014.

 

 

 

Show More

Related Articles