HabariMilele FmSwahili

Wakili Haron Ndubi akanusha mashtaka ya kuendesha gari akiwa mlevi

Wakili wa maswala ya haki za kibinadamu Haron Ndubi amekanusha mashtaka ya kuendesha gari akiwa mlevi na kufunga bara bara. Ndubi alikamatwa usiku wa kuamkia leo kwenye bara bara ya Jakaya Kikwete hapa jijini. Kamanda wa polisi Nairobi Japheth Koome alidhibitisha kuwa wakili huyo alikuwa mlevi alipokamatwa. Hata hivyo ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu 30. Kesi itasikilizwa Februari 23.

Show More

Related Articles