HabariMilele FmSwahili

Kesi ya kupinga ushindi wa gavana Ojaamong yatupiliwa mbali

Gavana wa Busia Sospeter Ojaamong amepata afueni baada ya mahakama kuu ya busia kutupilia mbali kesi ya kupinga ushindi wake katika uchaguzi mkuu wa Agsosti nane mwaka jana. Katika uamuzi wake jaji Kiarie Waweru amesema mlalamishu Peter Odima hakuwasilisha ushahidi wa kutosha kudhibitisha madai dhidi ya Ojamong. Odima ameagizwa kulipa tume ya uchaguzi IEBC na gavana Ojaamong shilingi milioni nne kila mmoja. Gavana Ojamong amepongeza uamuzi huo akisema utatoa fursa kwake kubuni baraza jipya la mawaziri wiki ijayo.

Show More

Related Articles

Check Also

Close