HabariPilipili FmPilipili FM News

Chama Cha KNUT Chapata Mwenyekiti Mpya Kilifi.

Jonathan Kenga sasa ndiye katibu mpya wa Chama Cha Walimu KNUT tawi la Kilifi , baada ya kuibuka mshindi kwenye uchaguzi wa chama hicho ulioandaliwa mwishoni mwa juma.

Kenga aliibuka mshindi baada ya kupata kura 576 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Matano Ayub Nasoro aliyepata jumla ya kura 366.

Akizungumza na wanahabari Kenga amewashukuru Walimu kwa kumchangua kuhudumu kwenye wadhifa huo kwa kipindi cha miaka 3, akiahidi kutekeleza majukumu yake ipasavyo kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wake aliyekuwa mpinzani wake wa Karibu Matano Ayub Nasoro amempongeza Kenga kwa ushindi huo, na kuahidi kushirikiana naye kufanikisha majukumu yao kwa walimu

Show More

Related Articles