HabariPilipili FmPilipili FM News

Kesi Ya Kupinga Uchaguzi Wa Spika Wa Kaunti Ya Taita Yawasilishwa Mahakamani

Spika wa bunge la kaunti ya Taita Taveta huenda akajipata katika njia panda kufuatia kesi ya kuharamisha uchaguzi wake wa awamu ya pili, kuwasilishwa katika mahakama kuu mjini Voi.

Wakiongozwa na aliyekuwa diwani katika kaunti hiyo Leonard Mwayongo, wanaharakati kadha wameiomba mahakama kufutilia mbali uteuzi wa spika wa kaunti ya hiyo Meshack Maghanga kwa madai ya kukiukwa sheria wakati wa zoezi hilo.

 

Kesi hiyo pia imemhusisha  katibu wa bunge la kaunti hiyo Michael Ngala kwa madai ya kutowajibika ipasavyo, kwa madai ya kumuidhinisha spika bila kuwa na cheti cha kulipa ushuru wakati wa kuchaguliwa kwake kama spika wa bunge la Taita-taveta.

Mashtaka hayo ni ya pili dhidi ya spika Maghanga baada ya kuondolewa mashtaka ya kupinga kuendeleza shughuli za bunge mwaka jana

Show More

Related Articles