
Ndugu, jamaa na marafiki wa waathiriwa wawili wa mkasa wa ndege aina ya helikopta iliyotumbukia ziwani Nakuru Oktoba mwaka uliopita, walikusanyika ufukweni mwa ziwa hilo na kufanya ibada ya kumbukumbu baada ya miili wa wawili hao kutopatikana.
Wawili hao Sam Gitau na John Ndirangu, walikuwa miongoni mwa watu watano walioaga dunia ziwani humo baada ya ndege walimokuwa wakisafiria kuanguka ziwani humo kufuatia hali mbaya ya anga.