HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

NCCK yataka Wakenya kukomesha cheche za siasa za uchaguzi

Baraza la makanisa nchini NCCK limewataka wakenya kumaliza msimu wa siasa na chaguzi za mwaka wa 2017 na kuwaleta kwa pamoja wahusika wakuu, ili kutia kikomo mihemko ya kisiasa ambayo imeligawanya taifa.
NCCK imesisistiza kuwa wakenya na viongozi wa mirengo tofauti lazima wabadilishe mwelekeo na kumaliza ubishi mkali ambao umekuwa ukionekana kati ya serikali na upinzani.
Vile vile baraza hilo limeonya dhidi ya matamshi ya kinara wa NASA Raila Odinga kutaka kuwa na uchaguzi kabla ya mwezi Agosti mwaka huu wa 2018 wakishikilia kuwa hili litaathiri nchi zaidi.

Show More

Related Articles