HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Kamati ya Bunge kuhusu uteuzi yakamilisha zoezi la kuwakagua

Mawaziri wapya walioteuliwa sasa wanasubiri kuidhinishwa au kutemwa na bunge la kitaifa baada ya kamati ya bunge kuhusu uteuzi kutamatisha zoezi la kuwapiga msasa jioni ya leo.

Kamati hiyo inayoongozwa na Spika wa Bunge Justin Muturi, inatarajiwa kwenda faraghani kule Naivasha kuandika ripoti ya ukaguzi huo ambayo itakuwa na mapendekezo kuhusu kila waziri aliyehojiwa.

Na kama anavyotuarifu Kiama Kariuki, huenda mapendekezo yatakayowaslishwa bungeni yakapokelewa kwa upinzani mkali kwani ni wanakamati kutoka chama cha Jubilee walioshiriki kuwahoji.

Show More

Related Articles