HabariPilipili FmPilipili FM News

Mahakama Ya Machakos Ya Tupilia Mbali Kesi Ya Kupinga Ushindi Wa Mutua

Gavana wa kaunti ya machakos Alfred Mutua amepata afueni hii ni baada ya mahakama kuu mjini Machakos kutupilia mbali kesi ya kupinga ushindi wake iliyowasilishwa na aliyekua mpinzani wake Wavinya Ndeti.

Akitoa uamuzi huo jaji Agrey Muchelule amesema hakukuwa na ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha kwamba uchaguzi wa agosti nane mwaka jana ulikuwambwa na dosari.

Muchelule amesema kuchaguliwa kwa Mutua ilikuwa ni maamuzi wa wakaazi wa Machakos.

Mahakama imemuamuru mlalamishi Wavinya Ndeti kulipa shilingi milioni 10 kwa IEBC na gavana Mutua kama gharama ya kesi hiyo.

 

Show More

Related Articles