HabariPilipili FmPilipili FM News

Hospitali Kuu Ya Kenyatta Ya Ingia Katika Vitabu Vya KumbuKumbu

Hospitali kuu ya Kenyatta imeandikisha historia kwa mara nyingine kanda ya Afrika Mashariki na mataifa yanayopakana na jangwa la sahara, baada ya kufanikiwa kufanya oparesheni ya kurejesha sehemu ya mkono ya kijana mmoja kutoka kaunti ya Kiambu.

Joseph Theuri mwenye umri wa miaka 17 kutoka eneo la Kiambaa katika kaunti hiyo alikatwa kiganja cha mkono wake na mashine ya kukata nyasi.

Upasuaji wa kurudisha mkono wake uliochukua saa 7 kukamilika, ulihusisha wahudumu wa afya 15 kutoka hospitali hiyo na chuo kikuu cha Nairobi.

 

Show More

Related Articles