HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

KNH yafaulu kufanya oparesheni kurejesha kiganja cha mkono

Hospitali kuu ya Kenyatta imeandikisha historia kwa mara nyingine tena Afrika Mashariki na mataifa yanayopakana na jangwa la sahara baada ya kufanikiwa kufanya oparesheni ya kurejesha sehemu ya mkono ya kijana mmoja kutoka Kiambu.

Joseph Theuri mwenye umri wa miaka 17 kutoka eneo la Kiambaa kaunti ya Kiambu alikatwa kiganja cha mkono wake na mashine ya kukata nyasi.

Upasuaji huo uliochukua saa 7 ulihusisha wahudumu wa afya 15 kutoka hospitali hiyo na chuo kikuu cha Nairobi.

Show More

Related Articles