HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Mawaziri watano kati ya 21 walioteuliwa wamehojiwa bungeni

Mawaziri watano kati ya ishirini na mmoja walioteuliwa na Rais Uhuru Kenyatta hii leo wamefika mbele ya kamati ya bunge kuhusu uteuzi, ambapo wamefanyiwa ukaguzi wa iwapo wako na uwezo wa kuhudumu katika wizara walizoteuliwa.

Wa kwanza kufika mbele ya kamati hiyo alikuwa waziri mteule wa huduma za umma Prof. Margaret Kobia, ambaye hadi uteuzi wake alikuwa mwenyekiti wa tume ya huduma za umma.

Prof. Kobia wakati wa ukaguzi wake alitetea hatua ya Rais Uhuru Kenyatta ya kuunda nafasi ya makatibu wasaidizi wa wizara ambapo alisema Kenyatta alifanya mashauriano ya kutosha na tume yake kabla ya hatua hiyo.

Show More

Related Articles