HabariMilele FmSwahili

Dr Monica Juma ahojiwa na kamati ya bunge kuhusu uteuzi

Uhusiano wa Kenya na mataifa mengi umeimarika zaidi chini ya utawala wa rais Uhuru Kenyatta. Dr Monica Juma aliyependekezwa kuhudumu kama waziri wa masuala ya kigeni anasema hilo limeafikiwa kutokana na sera bora za Kenya kuhakikisha ushirikiano bora na mataifa tofauti duniani. Dr Juma ambaye kwa sasa ni katibu katika wizara hiyo anasema lengo lake ni kuhakikisha mchango wa Kenya unatambulika zaidi katika mikutano ya kimataifa. Ametumia vikao hivyo kukumbuka yaliomkabili mwaka 2015 alipokataliwa na wabunge kuhudumu kama katibu kwa baraza la mawaziri akisema alisoma mengi kutokana na hatua hiyo.

Show More

Related Articles