HabariPilipili FmPilipili FM News

Uhaba Wa Maji Mombasa.

Wakaazi wa Kongowea eneo bunge la Nyali Kaunti ya Mombasa wanalalamikia uhaba wa maji kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa.

Wakizungumza na meza yetu ya habari hii leo, wakaazi hao wanasema wanalazimika kununua maji ya kisima kwa bei ya juu na ambayo sio safi na salama kwa afya yao.

Wafanyibiashara nao wanasema uhaba wa maji umeathiri biashara pakubwa.

Wanasema licha ya kulizungumzia suala la uhaba wa maji kwa viongozi waliowachagua, bado hawajapata suluhu yoyote.

Wengine wameitaka serikali ya kaunti ya Mombasa wachimbe visima ili wasaidike wakati kuna uhaba wa maji eneo hilo na wengine nao wakilalamikia mirundiko ya taka eneo hilo.

Juhudi zetu za kuongea na katibu wa maji kaunti ya Mombasa hazikufua dafu huku ikibainika kuwa uhaba huo wa maji umechangiwa na madeni yanayodaiwa kampuni za maji za kaunti za Pwani ikiwemo Mawasco, Tavevo na Kwawasco.

Show More

Related Articles