HabariPilipili FmPilipili FM News

John Munyesi Amepigwa Msasa Na Kamati Ya Bunge.

Waziri mteule katika wizara ya petroli na madini John Munyes amefika mbele ya kamati ya uteuzi bungeni ili kujitetea kabla ya kushikia wadhfa huo rasmi.

Akijibu maswali ya wanachama wa kamati hiyo. Munyes amesema atalipa kipau mbele suala la kushauriana na wananchi na wawekezaji kuhakikisha kila mmoja anafaidi na mali asili ya taifa hili.

Munyes ambaye kwa sasa anaendelea kuhojiwa na kamati hiyo, anasema kwa muda mrefu wananchi wametelekezwa katika kunufaika na bidhaa hizo na wakati umefika hilo kubadilika.

Aidha anasema lazima kuwepo sheria za kuwashinikiza wawekezaji kuwashirikisha kikamilifu kwenye shughuli ya uchimbaji madini na kupata mapato yake.

Amesema atahakisha leseni za uchimbaji madini zinatathiminiwa upya wakati akiingia afisini.

Show More

Related Articles