HabariMilele FmSwahili

Magari ya uchukuzi wa umma yatiwa mbaroni na bodi ya KFCB Mombasa

Zaidi ya magari 78 ya uchukuzi wa umma yanayohudumu ndani ya kaunti ya Mombasa pamoja na madereva na makanga wao  wametiwa mbaroni kufuatia msako ulioendeshwa na maafisa wa bodi ya kudhibiti filamu KFCB ikishirikiana na maafisa wa polisi dhidi ya magari yanayodaiwa kuonyesha filamu za ngono. Afisa mtendaje wa bodi hiyo eneo la Pwani Bonventure Kioko amesema magari hayo yameshikwa baada ya kupatikana yamekiuka sheria. Mkurugenzi mkuu wa bodi hiyo nchini Ezekiel Mutua ametoa wito kwa wamiliki magari ya umma kuchukua leseni zitakazotoa muongozo wa yale yanayofaa kusikilizwa na kuonyeshwa kwenye magari hayo.

Show More

Related Articles