HabariMilele FmSwahili

John Munyes afika mbele ya kamati ya bunge kuhusu uteuzi

Waziri mteule katika wizara ya mafuta na madini John Munyes anasema atalipa kipau mbele suala la kushauriana na wananchi na wawekezaji kuhakikisha kila mmoja anafaidi na mali asili ya taifa hili. Munyes ambaye wakati huu anahojiwa na kamati ya bunge kuhusu uteuzi anasema kwa muda mrefu wananchi wametelekezwa katika kunufaika na bidhaa hizo na wakati umefika taswira hiyo kubadilika. Aidha anasema lazima kuwepo sheria za kuwashinikiza wawekezaji kuwashirikisha kikamilifu kwenye shuguli ya uchimbaji madini na kupata mapato yake.

Show More

Related Articles