HabariPilipili FmPilipili FM News

Mshukiwa Wa Ugaidi Akamatwa Kilifi.

Maafisa wa polisi mjini Kilifi wanamzulia mwanamke mmoja raia wa taifa jirani la Somali wakimshuku alikuwa ana njama ya kutekeleza jaribio la ugaidi.

Akithibitisha kisa hicho mshirikishi wa usalama Kaunti ya Kilifi Elisha Ng’etich amesema, mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 44 ambaye alikuwa amevalia Buibui na Ninja amekamatwa na maafisa wa usalama waliokuwa wakishika doria katika benki za Posta, NIC na SMEP ambapo alikuwa akiingia benki moja hadi nyingine pasi kutoa wala kuweka pesa.

Kulingana na mshirikishi huyo, mshukiwa huyo hata hivyo kando na kupatikana  na paspoti kadhaa aidha amepatikana na Dola 881 za Marekani huku akiongeza kuwa hatua yake ya kususia kuongea imewafanya maafisa hao kumpeleka kwa maafisa wa jinai kwa uchunguzi  zaidi.

Kwa upande wake kamishina wa kaunti hiyo Magu Mtindika amesema mshukiwa huyo ataendelea kuhojiwa na maafisa wa jinai ili kupata habari kwa kina huku akiwataka wananchi kushirikiana na idara ya usalama ili kudhibiti vita  vya ugaidi kanda ya pwani.

Show More

Related Articles