HabariPilipili FmPilipili FM News

Kobia Apigwa Msasa Na Kamati Ya Bunge.

Margaret Kobia aliyependekezwa kuhudumu katika wizara ya utumishi wa umma vijana na jinsia amefika mbele ya kamati ya uteuzi hivi leo kupigwa msasa.

Kamati hiyo inayoongozwa na spika wa bunge la kitaifa Justin Muturi pia itawahoji John Munyes wa kawi, Monica Juma wa masuala ya nje na waziri mteule wa ardhi Farida Karoney.

Muturi amewahakikishi wakenya lalama zozote zilizowasilishwa dhidi ya wateule hao zitaangaziwa.

Zoezi la kuwapiga msasa wote hao litakamilika hapo kesho.

Show More

Related Articles