HabariPilipili FmPilipili FM News

Kilio Cha Wahudumu Wa Boda Boda Mtwapa.

Sekta ya uchukuzi wa boda boda mjini Mtwapa imeitaka serikali kuingilia kati na kuweka vigezo vitakavyo thibiti visa vya mauaji na wizi wa pikipiki ambao kwa sasa umekithiri kwa kiwango kikubwa.

Akizungumza na wanahabari mjini Mtwapa, katibu wa sekta hiyo mjini humo Armstron Mwangala maaruf Santa Bingo amesema ongezeko la wahudumu hao limechangia pakuwa visa hivyo kwa kuwa wengi wao ni watoto wadogo wakiwemo wa darasa la tano na hata la sita.

Ametaja a kwa kila kijiji takriban asili mia 75 ya vijana wanashiriki huduma ya boda boda jambo ambalo limepelekea wengi wao kuacha shule huku idadi ya wahudumu hao ikiwa zaidi ya 2000.

Hata hivyo katibu huyo amewataka wahudumu hao kujiunga  na chama cha wanabodaboda kilichoko mjini humo ili kuweza kupata mafunzo ya kukabiliana na visa hivyo.

Hadi kufikia sasa takriban pikipiki 20 zimeripotiwa kuibiwa na baadhi ya wahudumu kuuwawa  mjini humo.

Show More

Related Articles