HabariMilele FmSwahili

Kipsang :Wanafunzi katika shule za upili kupokea vitabu 6 vya masomo muhimu

Wanafunzi wote katika shule za sekondari watakuwa wamepokea vitabu sita vya masomo muhimu ifikiapo mwezi Julai mwaka huu. Katibu wa wizara ya elimu Dkt Belio Kipsang anasema seriklai itawafikishia wanafunzi wote vitabu vya masomo ya kingereza, kiswahili,hesabu, sayansi, kemia na bayolojia. Amesema serikali pia itaendelea kutoa mafunzo kwa walimu kuhusiana na utekelezwaji wa mfumo mpya wa elimu. Naye katibu mkuu wa tume ya kuwaajiri walimu dkt Nancy Macharia amesma tume hiyo itafanyia mabadiliko mfumo wa kuwajiri na kuwatuma walimu ili kukabiliana na uhaba wa walimu kwenye maeneo kame.

Show More

Related Articles

Check Also

Close