MakalaMilele FmSwahili

Margret Kobia aanza kuhojiwa na wabunge

Zoezi la kuwapiga msasa wakenya 9 waliopendekezwa na rais Uhuru Kenyatta kuhudumu kwenye baraza la mawaziri linaendelea wakati huu katika majengo ya bunge. Zoezi hilo linaongozwa na spika wa bunge aliye pia mwenyekiti wa kamati ya uteuzi ambaye ametangaza hakuna mkenya yeyote ataruhusiwa kufika mbele yao na kwamba watazingatia tu hati viapo walivyopokea kutoka kwa wananchi kufikia jana jioni.
Profesa Margret Kobia alyependekezwa kuhudumu kama waziri wa masuala ya vijana, jinsia na utumishi wa umma anakaguliwa wakati huu ambapo ameelezea kujitolea kwake kuhudumu kwneye wadhfa huo

Show More

Related Articles